Pages

Subscribe:

Saturday, December 23, 2017

JUX AMPIGA MARUFUKU G NAKO KUINGIA KWENYE CHUMBA CHAKE NA MPENZI WAKE



STAA wa muziki kutoka WEUSI Kampuni Tanzania, G Nako ameonesha mshawasha wa kukitamani chumba ambacho Jux amekitangaza kuwa kitakuwa ni maalum kwake na Baby yake.

Kupitia mtandao wa Instagram Jux alitangaza kuwa amekamilisha chumba cha studio ambacho amekiweka mbali na kazi za kibiashara na kukitaja kuwa atakitumia yeye na baby yake pekee na kumtaka G Nako...
asijilete lete katika studio hiyo.
 
G Nako kuona kapewa sharti hilo, hakukaa kimya kabisa bali aliutumia uwanja wa maoni katika post hiyo na kuandika ‘Hahahahaha kiandeeee utanikutaa kwenyee poool natafutaa melodies mzeeee @juma_jux”.

Hata hivyo mpaka sasa haijaelelweka ni Baby yupi ingawa kila mara tumekuwa tukigundua kuwa karibuni hasa Jux amekuwa akimuita Vanessa Mdee’ Baby na hilo kama litakuwa na ukweli basi Vanessa atakuwa ametengua kauli yake ya kuwa haweza kurudiana na mtu ambaye ameachana naye kimahusiano.

0 comments:

Post a Comment