Pages

Subscribe:

Monday, December 25, 2017

STORY: NALIA NA NAFSI YANGU (Sehemu Ya 12) - 12

Related image
Sehemu ya:12 
Mtunzi: Agatha Francis
 
" Hapana bado sijamnyonyesha nesi"alijibu mkewe Baraka kisha nesi aliagiza amnyonyeshe vizuri, basi mkewe Baraka alitii agizo la nesi nakuanza kumnyonyesha mwanae, alipokua akimnyonyesha alimuuliza mume wake"mume wangu mbona mtoto mdogo hivi", Baraka akajibu usijali mke wangu ukimaliza tu mnyonyesha mtoto inabidi tuonane na daktari, sawa alijibu mkewe huku akiendelea mnyonyesha mwanae kwa wasiwasi. 

Alipomaliza nyonyesha alijiandaa kwaajili yakukutana na daktari, basi Baraka alimuhudumia mke wake vizuri kisha kwenda kuonana na daktari, walipofika daktari aliwapongeza sana lakini...
alisisitiza kuhusu suala na kumnyonyesha vizuri mtoto kwani afya yake haikua nzuri sana, wote walikubaliana na daktari na baadae waliruhusiwa na kuanza safari ya kurudi nyumbani. Mkewe Baraka alimtanda mwanae nguo nyingi ili aweze kumbeba vizuri maana mtoto alikua mdogo si kawaida. 

Hali ile ilimkosesha amani kabisa alikua akiwaza sana kiasi kwamba mume alilitambua hilo na kumpa mke wake moyo kwa kusema "mke wangu jitahidi tu kufuata maelekezo ya tabibu, pia ule vizuri bila shaka atakua vizuri kabisa", sawa mume wangu lakini mmmh", aliguna mkewe kwani alihisi uenda mwanae akapoteza maisha. 

Basi walifika nyumbani na maisha yaliendelea kama kawaida,watu walienda kuwaona kama ilivyo kawaida na mzee Moto pia alienda kuwaona hali iliyowafanya washangae kwani kwa ugomvi ambao ulikuapo kati yao haikua rahisi kwa mzee huyo kwenda kuwaona, walihisi amesha samehe na maisha yaendelee. 

Maneno ya chinichini yalisikika mengi sana kuhusu mtoto yule aliyezaliwa ambae walimuita Prisca, kila mtu aliongea lake maana alikua mdogo mno, alivalishwa soksi nyingi ili mradi kumuongezea ukubwa, alifunikwa kwa nguo nyingi sana ili tu aonekane mkubwa. 

Maskini mama Prisca mke wa Baraka hakua na amani tena alishinda akiudhunika tu kuhusu mwanae watu walimshauri kumnyonyesha lakini haikusaidia kitu hali ilizidi kua mbaya. Kitu kilichomchanganya sana mama Prisca ni homa zisizoisha kwa mwanae huyo na kila alipoenda hospitali alipewa dawa za maumivu lakini mtoto alipopimwa hakuonekana na tatizo lolote. Je unadhani nini shida,?

usikose 13

0 comments:

Post a Comment