Pages

Subscribe:

Sunday, December 31, 2017

WARUSI WAMFANYA DKT SHIKA KUKACHA DILI ZA KUFANYA MATANGAZO


Mtanzania Dkt. Louis Shika aliyejizolea umaarufu mkubwa hivi karibuni katika mitandao na vyombo vya habari ameeleza sababu ya kuacha kufanya matangazo ya kibiashara na kampuni mbali mbali.

Dkt. Shika amekiambia kipindi cha Weekend kuwa ameacha kufanya matangazo kwa kuhofiwa kufuatiliwa na maadui zake kutoka nchi ya Urusi alipokuwa...
akifanya kazi miaka ya nyuma.

“Sina interest na haya matangazo tena kwa sababu wale Warusi niliowakimbia watani-track watajua niko wapi, lakini natoa ushirikiano kwa wenzangu huku nikiwa nimetafuta means nyingine za kuwakwepa,” amesema Dkt. Shika.

Dkt. Shika ameweza kufanya tangazo la kampuni moja ya michezo ya ubashiri matokeo katika soka, pia ameweza kuonekana katika video mbili za nyimbo za Bongo Flava. Video hizo ni za Kundi la Rostam ‘Kiba_100’ na wimbo wa Gaza ‘Nanii’ akishirikiana na Madee.

0 comments:

Post a Comment