skip to main |
skip to sidebar
AFYA: HIZI NDIYO NJIA KUU 8 SALAMA ZA KUPUNGUZA MATITI
kawaida matiti huanza kutokea na kukua pale mwanamke anapokua amevunja
ungo, ukubwa huu husabishwa na kuanza kumwagika kwa kiasi kikubwa cha
homoni za uzazi yaani oestrogen, kuongezeka na kupungua kwa matiti
hutegemea sana kiasi cha homoni kinachopanda na kushuka kila siku kwenye
mwili wa mwanamke ndio maana kuna tofauti kidogo ya ukubwa wa matiti
siku za kawaida za mwanamke na kipindi cha hedhi.
matiti yakiwa makubwa sana humnyima mwanamke raha kabisa na hupata
matatizo ya kisaikolojia hasa anaposhindwa kuvaa nguo nzuri na kukosa...
ujasiri mbele za watu,upele na fangasi chini ya matiti, maumivu ya
mgongo, maumivu ya shingo na kupumua kwa shida wakati wa kulala.
sasa unapoamua kupunguza ukubwa wa matiti kuna njia mbalimbali hutumika kuyapunguza matiti kama ifuatavyo.
upasuaji; hii ndio njia ya haraka ya kupunguza matiti na ni
salama sana kama ikifanyika na daktari mzoefu wa hizi kazi...kwa nchi
ambazo zimeendelea pasuaji hizi zinapatikana sana na zaidi ya 99% ya
wanawake waliofanyiwa waliridhika na matokeo.
upasuaji huu hufanyika kwa kupasua matiti na kuondoa sehemu kubwa ya
mafuta inayopatikana kwenye matiti kisha chuchu hukatwa vizuri na
kuwekwa sehemu mpya ili iandene na matiti mapya, changamoto kubwa ya
upasuaji huu ni gharama na haipatikani hapa nchini.
mazoezi; ukiwa na matiti makubwa hakikisha uko kwenye uzito
sahihi kwani kama wewe ni mnene basi unene wako pia unachangia kwenye
ukubwa wa matiti yako, hivyo anza mazoezi ya mwili mzika kama kukimbia,
kuendesha baiskeli, fanya mazoezi ya aerobics[hufanyika kwa mziki kwenye
gym mbalimbali].ukianza kupungua uzito basi sehemu kubwa ya matiti yako
pia itapungua ukubwa uzito. kumbuka kuvaa sidiria inayobana sana wakati
wa mazoezi ili usisumbuke.
massage; kwa kutumia njia hii hakikisha kila titi unalipa muda
sawa wa kulifanyia masaji ili yote yaweze kupata matokeo sahihi, chukua
mafuta ya olive oil mwaga kidogo kwenye titi na uanze kulifanyaia masaji
kwanzia katikati huku unazunguka kama duara mpaka pembeni kabisa ya
titi. kila titi lifanyia masaji kwa dakika kumi mara mbili kwa siku na
matokeo huanza kuonekana angalau baada ya miezi mitatu.
tangawizi; hii ni njia ya asili sana ya kupunguza matiti hata
kwenye jamii za zamani...tangawizi huongeza kasi ya mwili kuchoma mafuta
pia na kupunguza mafuta yapatikanayo kwenye matiti.
jinsi ya kutumia;
chukua kijiko cha chai kilichojaa tangawizi ya unga kisha chemsha na
kikombe kimoja cha chai kwa dakika kumi, kisha mimina kwenye kikombe na
changanya na kijiko kimoja cha asali. kunywa vikombe viwili mpaka vitatu
kwa siku.
green tea; haya ni majani ya chai ambayo yanapatikana sehemu
mbalimbali nchini kwa sasa, majani haya yanaongeze kasi ya mwili kuchoma
mafuta na hata kushambulia mafuta ya kwenye matiti.
jinsi ya kutumia;
weka majani ya chai kwenye kikombe chenye maji ya moto, funika kwa
dakika tatu mpaka tano, ongeza kijiko cha asali.kunywa vikombe vitatu
mpaka vinne siku.
mayai na limao; yai na limao pia ni bidhaa zinazotumika kupunguza
ukubwa wa matiti na kufanya yawe magumu yaani kitaalamu kama tonicity,
sasa chukua sehemu nyeupe ya yai na upake kwenye matiti na uache kwa
dakika 30 kisha chukua limao changanya na maji na utumie mchanganyiko
huo kusuuza matiti yako.
fanya hivyo mara moja kwa siku.
virutubisho vya fish oil; vidonge hivi hutengenezwa kwa mafuta ya
samaki, mafuta haya yana omega 3 ambayo kazi yake ni kuweka kiwango cha
homoni za oestrogen mwilini katika kiwango sahihi, kama nilivyosema
hapo mwanzo kiwango kikubwa cha homoni hii ni moja ya chanzo kikuu cha
matiti makubwa.kidonge kimoja kwa siku kinatosha sana.
Acha kutumia njia za uzazi wa mpango za dawa; njia pekee ya uzazi
wa mpango ambayo haitumii homoni ni kitanzi cha copper ambacho huwekwa
kwennye kizazi hivyo ni salama, dawa zingine zote, sindano na vijiti
zina homoni ambazo huchangia kuongezeka kwa ukubwa wa matiti.
mwisho; ni njia ya upasuaji tu yenye majibu ya haraka, njia hizi
zingine zinahitaji nidhamu na uvumilivu kwani matokeo yake yanachukua
muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment