Pages

Subscribe:

Saturday, November 4, 2017

ASLAY AUDANGANYA UMMA ILI KUMSAPOTI RAFIKI YAKE KIPENZI


Msanii wa muziki wa kizazi kipya na mkali wa ngoma ‘Natamba’ Aslay ameonekana kuwa msanii aliyediriki kuwadanganya mashabiki kwa mgongo wa ndoa kama njia pekee ya kuutetea ujio wa kazi mpya ya msanii mwenzake Enock Bella.

Oktoba 23 mwaka huu wa 2017, Aslay aliutumia ukurasa wake wa Instagram kuwadanganya mashabiki kwa bashasha za pongezi kwa hatua ya msanii mwezake Enock Bella kuchukua...
jiko(Yaani kupata mke/Kuoa). Katika picha Enock alionekana akiwa ni mwenye kujistili kwa suti ya gharama akiwa kamkaribiria mrembo mmoja kwa jina maarufu ‘Mami’ aliyejipamba kwa nakshi ya vazi la heshima mithiri ya Bibi Harusi.

Kilichokuja kugundulika usiku wa kuamkia tarehe 3 ya mwezi Novemba, Enock ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Sauda’ uliotayarishwa chini ya Studio za WCB Wasafi kwa mkono wa Lizer Classic huku video ikiongozwa na Director Ivan ambapo mrembo aliyetumika katika video hiyo ndo yule ambaye alitajwa kama mke wa Enock Bella katika picha aliyopost Aslay mrembo akiwa sambamba na Enock Bella.

Hata hivyo kingine ambacho kimetambulishwa rasmi kwa wengi ambao wanamfahamu na kumfatilia Enock Bella ni kusikika akijiita Enock Bella ‘Base’ kutokana na haina ya sauti anayoitumia katika uimbaji wake.

0 comments:

Post a Comment