Pages

Subscribe:

Wednesday, November 15, 2017

AT AFUNGUKA BAADA YA KUSHINDA TUZO MBILI NCHINI MAREKANI



Msanii wa muziki Bongo, AT ameweka bayana jina la tuzo alizoshinda alfajiri ya leo nchini Marekani. 

Akiongea kutokea nchini Marekani, mkali huyo wa miondoko ya duara alianza kwa kuwashukuru Watanzania kwa kumpigia kura kisha akabainisha kuwa tuzo hizo alizo mbili alizoshinda  haziitwi B&K bali zinaitwa Mama Awards na B&K ni...
kampuni walishirikiana kuanda tuzo hizo.

“Nataka niweke wazi hizo tuzo haziitwi B&K, hizi tuzo zinaitwa Mama Awards na kuna tofauti kati ya Mama Awards na Mama Award. B&K ni kampuni ama watu walioshirikiana kuweza kuandaa tuzo hizo.

Akaongeza “Tuzo hizi zilikuwa kwa muda mrefu na mimi nimewashtukiza Watanzania kuwaambia kwa sababu nimetumia akili za kuzaliwa. Wakati watu wanaanza kupiga kura sikuwa nimewaambia mimi Watanzania, nimewaamia karibu na mwisho”.
AT ameshinda tuzo mbili ambazo ni ‘International Artist’ na ‘Best Music Video’

0 comments:

Post a Comment