Pages

Subscribe:

Friday, November 10, 2017

DIAMOND AFUNGUKA SABABU YA KUACHIA ALBUM KIPINDI HIKI


Msanii wa muziki Bongo, Diamond Platnumz amefunguka mambo kadhaa kuhusu ujio wa albamu yake mpya ‘A Boy From Tandale’.

Muimbaji huyo amesema albamu hiyo anaihesabu kama ya kwanza kwake kutoka amejaribu kuweka hisia zake zote huku akieleza sababu ya kutoa albamu hiyo kipindi hiki ambacho hakuna...
soko la uhakika.

“Nafikiri ni kutokujua ni njia ipi utumie katika kuuza albamu kwa sababu ukitumia tu kwenye CD siku hizi hamna mtu anatumia CD, sasa hivi ni digital unaweza kuuza katika mitandao mikubwa na watu wanaweza kununua, vile vile inakutengeneza misingi mikubwa” amesema.

“Kama mimi ni msanii ambaye kwa wiki naweza kutunga nyimbo mbili kwa hiyo nisipotoa albamu nitakuwa na nyimbo nyingi ndani ambazo zitakufa” Diamond ameiambia BBC Swahili.

Wasanii wa Bongo Flava ambao wametoa albamu kwa mwaka huu ni pamoja na Lady Jaydee, Navy Kenzo, Chege, Ben Pol na wengineo.

0 comments:

Post a Comment