Pages

Subscribe:

Monday, November 13, 2017

ENOCK BELLA: SAUTI YANGU HAIWEZI KUNIKWAMISHA NAWEZA KUIBADILI


Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Enock Bella amesema sauti yake inaweza kufanya chochote katika muziki.

Muimbaji huyo ambaye alijichotea umaafufu mkubwa katika kundi la Yamoto Band kwa kuimba sauti ya bezi amesema hilo haliweza kumkwamisha kipindi hiki ambacho anafanya muziki pekee yake kwani...
ana uwezo wa kubadilisha (switch) sauti hiyo.

“Sauti yangu inaweza kufanya kitu chochote, halafu nimejua kwamba kupitia sauti yangu ya bezi naweza kutengeneza muziki ambao unaishi ndio maana nikafanya kitu kikubwa kama hiki” amesema Enock Bella.

Kwa sasa Enock Bella anatamba na ngoma yake mpya ‘Sauda’ ikiwa ni ya kwanza kutoa tangu kuacha kufanya kazi na Yamoto Band.

0 comments:

Post a Comment