Pages

Subscribe:

Thursday, November 9, 2017

IDADI YA WANAFUNZI WALIO FARIKI KWA BOMU HUKO KAGERA YASIKITISHA WENGI

Wanafunzi 9 wa shule ya msingi Kihinga mkoani Kagera wamefariki dunia na wengine zaidi ya 25 kujeruhiwa baada ya kulipukiwa na bomu. 

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kagera Agustino Olomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema kwamba wanafunzi hao walikuwa wakati wa mapumziko ya saa nne, na ndipo mlipuko huo ulipotokea na...
kusababisha madhara makubwa ya vifo.

Kamanda Olomi amesema tayari wananchi wamejitokeza kuchangia damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi.

Kwa mujibu wa Dokta Mariagoreth Fredrick ambaye ni mganga mkuu hosipitali ya Rurenge, amethibitisha kupokea miili hiyo na majeruhi ambao baadhi wako katika hali mbaya na tayari wanapatiwa matibabu.

"Tulionao hali ya sio nzuri. Wengine wameumia matumbo, wengine wamechanika bandama, wengine wamevunjika miguu, wengine vichwa vimepata maijraha, wengine wameumia macho", amesema Dokta Mariagoreth.

Inaelezwa kwamba kabla ya kulipukiwa na kifaa hicho kinachoarifiwa kuwa ni bomu, wanafunzi hao walikuwa wanakichezea bila kujua ni hatari.

0 comments:

Post a Comment