Pages

Subscribe:

Saturday, November 4, 2017

MAITI YA TRUMP KUONEKANA KWENYE COVER LA ALBUM YA SNOOP


Rapper mkongwe wa Marekani, Snoop Dogg ameonesha cover la album yake mpya, “Make America Crip Again.” Picha hiyo inaonesha kile kinachoonekana kuwa ni maiti ya rais wa Marekani, Donald Trump ambayo imefunikwa bendera ya Marekani. 

Kwenye picha hiyo ambayo tayari ameitoa Instagram, inamuonesha rapper huyo akiwa na kikombe na akiangalia mwili huo ambao...
kwenye kidole gumba umewekewa label yenye jina ‘Trump.’ Picha hiyo inafanana na album ya mwaka 1991 ya rapper Ice Cube, “Death Certificate,” ambapo mwili wake umeandikwa “Uncle Sam.”

Mapema mwaka huu Snoop aliachia wimbo “Lavender,” ambao kwenye video hiyo anaonekana akitumia bunduki bandia kumpiga mwanasesere mwenye sura ya Trump.

0 comments:

Post a Comment