Pages

Subscribe:

Monday, November 13, 2017

YOUNG KILLER NA DAVIDO WAHUSIKA KWENYE ALBUM YA DIAMOND



A Boy From Tandale ni moja kati ya albamu ambayo inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki. Diamond amewataja wasanii wengine ambao watasikika kwenye albamu hiyo. Akiongea na mtangazaji wa BBC Swahili, Salim Kikeke, hitmaker huyo wa Halellujah amewataja wasanii hao kuwa ni Young Killer na Davido kutoka Nigeria.

“Nimewashirikisha wasanii tofauti tofauti japo kuwa wengine naogopa kuwataja ili isife. Kuna msanii kama Young Killer nimefanya nae kutoka nyumbani Tanzania, Nigeria nimefanya na Davido. Wote...
watakuwepo kwenye albamu yangu hii mpya ‘A Boy From Tandale’,” amesema Diamond.

Bosi huyo wa WCB ameongeza kuwa wimbo wake ambao amemshirikisha rapper Rick Rose kutoka marekani utakao toka Disemba 1 ya mwaka huu unaitwa ‘Waka’.

0 comments:

Post a Comment