Sehemu ya:5
Mtunzi: Agatha Francis
Baraka ambaye ni mume wake hakupendezwa na
swali lile aliinuka nakuingia ndani, alipofika ndani alikuta Mark
kajiinamia analia, aliumizwa na maneno ya dada yake kiasi kwamba
alishindwa kuzuia machozi. Baraka aliumia sana kumuona shemeji yake
katika hali ile kwani Mark alikua kijana mpole mstaarabu ambae hakua
muongeaji sana.
Alipomuona Mark akasema"shemeji umemuacha na nani Nancy
wangu", maana dada anaweza akafanya jambo la ajabu huko nje, Baraka
alitikisa kichwa kisha akasema...
"pole sana shemeji yangu, mpenzi wako
kaondoka kwani alishindwa vumilia, alipofika hapo Mark aliinuka nakusema
kwanini umemruhusu jamani?, nitaiweka wapi sura yangu mimi.
Mwanamke
yule kabadilisha tabia zangu leo dada ananifanyia hivi jamani, alilia
sana, Baraka aliona hudhuni ya shemeji yake alimkumbatia akimbembeleza
anyamaze kwani anaweza jiletea ugonjwa. Mke wa baraka alisikia kelele
zile ndani, roho ilimuuma kwani alimpenda kaka yake hivyo akaingia ndani
nakusema nisamehe kaka yangu mimi nilikua nakukumbusha tu wazazi
walivyosema, huwezi oa mjini, alisema hayo huku sura ikionesha hamaanishi
anachosema, haya nyamaza kaka yangu, nyamaza mdogo angu twende kwa
mwenyekiti, huyo mama Careen atafika tu huko kwenu ila utaondoka na
Suzan alisema hayo huku akiwavutia nje.
Baraka alikua bado kamshikilia
shemeji yake Mark kwani Mark bado hakua vizuri, Mark alimuangalia dada
yake kisha akasema"nashukuru sana dada yangu kwa upendo wako mimi nitaoa
mwanamke ambaye mlimtaka wewe na wazazi ila kamwe siwezi muacha mama
Careen", dada alicheka kisha akasema nashukuru umenielewa utajua wewe na
wanawake zenu wa mjini matapeli tu mke Suzi bhana na akijua umekuja
atafurahi huyo, haya twendeni, alitoka nje nakuawaacha Baraka na shemeji
yake.
Baraka akasema pole sana Mark, Mungu mwema atakusaidia ila kama
mama Careen anamapenzi ya kweli kwako kwa hali aliyoiona atakuelewa tu,
kwasasa twende kwa mwenyekiti kwanza tukirudi huko tutaongea zaidi sawa
shemeji, Mark alishusha pumzi kisha akasema nashukuru shemeji, ila
ntamuambia nini mama Careen anielewe mimi jamani, kanifanyia mengi yule
mwanamke, hapana shemu maisha yangu nina hakika yatakua magumu.
Usikose sehemu ya 6
Click hapa unifollow instagram SmashJuanito
Saturday, December 2, 2017
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment