Mwalimu na mwanamuziki wa bongo Fleva, Barnaba Elias 'Barnaba Classic'
amefunguka na kudai anam-miss sana mama Steve 'Zuu Namela' japokuwa kwa
sasa hayupo tayari kumrudia mzazi mwenzake huyo.
Barnaba
ameeleza hayo baada ya kupita muda mrefu tokea aachane na mzazi
mwenzake huyo na kupelekea...
kuwa single mpaka kipindi hiki.
"Sitaweza kurudiana na mama watoto wangu japo nam-miss sana", amesema Barnaba.
Aidha, Barnaba amesema kwa upande wake
mapenzi hayajawahi kumuendesha hata kidogo kama baadhi ya watu wengine
wanavyokuwa baada ya kuachana na wapenzi wao kwa kushindwa hata
kuendelea kufanya kazi zao.
"Niwe mkweli tu, mimi
sijawahi kuendeshwa na mapenzi au mahusiano. Mapenzi hayana nafasi kubwa
katika maisha yangu japokuwa yana nguvu kwa mtu yeyote yule, mapenzi
hayajawahi kuchukua asilimia kubwa ya maisha yangu, kuniathiri wala
kunitikisa", amesema Barnaba.
Pamoja na hayo, Barnaba ameendelea kwa kusema "Kila
unachokiona kinatokea katika maisha yako kiwe kizuri au kibaya ni
mapito tu, kwa sababu kilichotuleta duniani ni kingine na tunachokifanya
ni kingine kwa hiyo muda mwingine kutendwa na vitu vingine ni kutenda
dhambi zaidi 'so sometimes' unatakiwa upokee kwa furaha chochote
utakachokumbana nacho katika maisha yako, kwa sababu hujui mpango wa
Mungu ukoje. Ninachoamini mimi ni kwamba nilikuwa napita kwenye daraja
ili niweze kuendela na safari aliyopanga Mungu 'so' sijui 'next'
nilichopangiwa na Mwenyezi Mungu", amesisitiza Barnaba.
Kwa upande mwingine, Barnaba japo
wameachana na Zuu lakini bado wanamawasiliano mazuri baina yao na kudai
hivi karibuni aliongea naye kuulizia maendeleo ya Steve ya kimasomo na
kumtumia pesa kwa ajili ya matumizi ya shule.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment