
Giligiliani
ni kiungo cha kawaida sana,wengi tunakitumia jikoni kwenye mapishi
mbalimbali,Kinaharufu nzuri na ladha ya uchachu kwa mbali. Majani na mbegu za
giligiliani vyote hutumika kama viungo jikoni.
Giligiliani
inawingi wa Vitamini A,B6,C,B12,pia ina wingi wa madini chuma(iron),Calcium
na Magnesium Giligiliani
inasifika kwakua dawa na kinga ya... magonjwa mengi. Historia inaonyesha kwamba
Kiungo hiki kilitumika kama dawa tangu enzi za kale nchini Egypt.Hata
hivyo,tafiti za kisayansi za karne hii ya 21 zinathibitisha taarifa hizi

Ni vyema kujua kwamba tunaposema chakula Fulani ni dawa,basi
maana yake ni kwamba chakula hicho kinavirutubisho Fulani ambavyo huweza kukabiliana na ugonjwa Fulani au laa kuupa mwili uwezo wa kukabiliana na kujikinga na ugonjwa Fulani na si vinginevyo.
Hizi ni baadhi ya faida za giligiliani katika afya :
1. Inawezesha usagaji mzuri wa chakula mwilini,hutuliza
tumbo na huondoa gesi kwenye utumbo mwembamba ambayo mara nyingi husababishwa na vyakula tunavyokula hivyo hupunguza utoaji gesi chafu (kunyampa) kwa kiasi kikubwa sana.
2. Inazuia magojwa ya tumbo yasabaishwayo na bacteria aina ya Salmonella.moja ya magonjwa haya ni kuumwa tumbo na kuhara.
3. Inazuia Ugonjwa wa (UTI.) Yaani Urinary tract infection
4. Inazui kutapika na hali ya kuvurugika tumbo
5. Inaondoa gesi tumboni
6. Inashusha sukari kwenye damu.(lower blood sugar)
7. Inapunguza cholesterol mbaya mwilin
8. Chanzo kizuri cha nyuzi nyuzi zinazoitajika mwilini ili
kuwezesha usagaji mzuri wa chakula (Dietary fiber)
9. Inawafaa sana wanawake ambao hupata hedhi nzito
10.Inaondoa maumivu,muwasho,na uvumbe(antinflammatory)
11. Huondoa chunusi na madoa kwenye ngozi Unaweza kuandaa giligiliani katika njia mbalimbali ili kuitumia kama dawa.
chemsha kijiko 1 cha chai cha mbegu za giligiliani na maji vikombe viwili. Chuja kisha ongeza sukari kidogo. Kunywa ikiwa yamoto au Maji ya vuguvugu Kuondoa maumivu (Inflamation) chemsha kijiko kimoja cha chai cha mbegu za giligiliani zilizosagwa na maji kikombe kimoja.Chuja kisha kunywa ikiwa vuguvugu.
Kunywa chai ya giligiliani (mbegu) mara kwa mara, pia tumia mbegu na majani ya giligiliani kwa wingi kwenye chakula.
Twanga au sigina majani ya giligiliani, chuja au kamua ili kupata maji yake. Pima vijiko vinne vya maji ya giligiliani kisha changanya na kijiko 1 cha chakula cha manjano(Binzari manjano).pakaa kwenye ngozi, acha ikauke kisha osha au nawa na maji vuguvugu. Onyo:usisugue ngozi
Changanya vijiko 2 vya chai vya maji ya giligiliani na kikombe kimoja cha maziwa fresh ambayo hayajatolewa krim Chai ya giligiliani (mbegu) husaidia kuondoa au kutuliza asidi tumboni.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment