Pages

Subscribe:

Tuesday, September 12, 2017

JAYDEE: NYIMBO ZANGU ZINAWEZA KUISHI HATA KWA MIAKA 10


JIBU LA SWALI NO. 3

Wasanii watatu walioshiriki kukamilisha huu wimbo mpya ni 
@jidejaydee - VERSES 2 za kuimba 
@onetheincredible - RAP VERSE 
@dkayafellow19 - CHORUS 
Lady Jaydee , One The Incredible na Domokaya 
Muhimu kutoa credit panapostahili, sio unashirikiana na watu kufanikisha jambo halafu unajidai kuwa ni idea yako peke yako unawanyima wenzio credit . 🙄🙄🙄🙄 Sio vizuri 
Ila hawa wananijua dada yao sio mchoyo wa kutoa credit wala nini 
Tupewe hongera zetu basi kabla hamjauskia wimbo
Watag na uwape hongera machizi wangu kwa kufanikisha hili

Kwenye kuandika huwa tunatumia kizungu kwahiyo itasomeka hivi:

Song written by: Lady JayDee, Domokaya & One The Incredible 
Producer nitakuja kumsifia kivyake kwakuwa hahusiki kwenye jibu la hili swali atawachanganya na hivi hampendi kusoma maelezo hamkawii kusema nimewaibia majibu

Washindi watatangazwa baada ya hii post ,..... pia @ladyjaydeediary kuna post ambazo haziko humu sitatajirika mki follow ila mtakosa mambo kwa ujeuri wa kuto follow😆😆😆😆😆😆

Msanii mkongwe wa bongo fleva, Lady Jay Dee maarufu kama 'Komando Jide" amefunguka na kudai haoni sababu ya yeye kutoa wimbo mpya kila mara kwa madai nyimbo zake ni za hisia ambazo zinaweza kuishi miaka mingi.

“Siwezi kutoa nyimbo mpya kila siku, kwa sababu nyimbo zangu ni za hisia, ambazo zinaweza kuishi hata miaka 10. Ni bora nitoe wimbo mmoja kwa mwaka lakini...
uwe unaishi miaka mingi kwa ladha ile ile siku zote," amesema Jay Dee.

Pamoja na hayo, Jay Dee amesema wasanii wengi wa kike wanashindwa kupambana katika muziki kutokana na kutopewa ushirikiano wa kutosha katika kile wanachokifanya japokuwa muda mwingine uongozi nao unachangia.

Lady Jay Dee ameachia ngoma ya 'I miss you' iliyotengenezwa na 'producer' Man water.

0 comments:

Post a Comment