Msimu wa UEFA 2017/18 umeanza rasmi usiku wa kuamkia leo kwa michezo
nane kupigwa huku mambo mbalimbali yakijitokeza zikiwemo rekodi kwa
baadhi ya timu pamoja na wachezaji.
Nyota
wa Barcelona Lionel Messi kwa mara ya kwanza amefanikiwa kumfunga
golikipa wa Juventus Gianluigi Buffon baada ya...
kufunga mabao mawili
katika ushindi wa Barcelona wa mabao 3-0. Katika mchezo huo Buffon
ametimiza michezo 117 ya UEFA.
Manchester United walikuwa wanarejea
kwenye michuano hiyo baada ya kuikosa msimu uliopita na mshambuliaji
wake mpya Romelo Lukaku ameingia kwenye orodha ya wachezaji waliofunga
katika mchezo wao wa kwanza wa UEFA baada ya kupachika bao moja dhidi ya
FC Basel.

Muunganiko wa washambuliaji wa PSG
Mbappe, Cavan na Neymar wanaounda 'MCN' wameendelea kufumania nyavu kwa
pamoja baada ya kuilaza Celtic 5-0 huku Kylian Mbappe akiweka rekodi ya
kuwa mchezaji mdogo zaidi kufikisha mabao 7 katika michuano hiyo.
Chelsea kwa mara ya kwanza imefunga
mabao 6 chini ya kocha Antonio Conte baada ya kuifunga Qarabag mabao
6-0. Bayern Munchen wameweka rwekodi ya kushinda michezo 14 mfululizo ya
ufunguzi wa hatua ya makundi.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment