Pages

Subscribe:

Tuesday, November 7, 2017

BEST NASSO: SASA NISHAKUWA MSANII WA MJINI


Msanii wa muziki Bongo, Best Nasso amesema si sawa kuitwa msanii wa kijijini kwani hata mjini anafanya vizuri pia. Muimbaji huyo amesema kuwa bado anaamini katika uwezo wake wa kimuziki ila suala la management ndilo limemkwamisha.

“Kilichokuwa kinanikwamisha ni kwa sababu mara ya kwanza nilikuwa na management na sasa hivi nipo nje ya management ndio utofauti mkubwa lakini Nasso ni yule yule na bado...
anafanya ngoma kali, nishakuwa msanii wa mjini” amesema Best Nasso.

“Sitaki kuamini mimi ni msanii wa kijijini pake yake lakini kama mjini wananifahamu mimi ni msanii wa kote kote, lakini kijijini nimekuwa na nafasi kubwa na mshindo mkubwa kuliko town” ameongeza.

Kwa sasa Best Nasso anatamba na ngoma yake mpya ‘Tumenatana’.

0 comments:

Post a Comment