Pages

Subscribe:

Tuesday, November 14, 2017

IDRIS SULTAN: KANUMBA ULIKUWA HUNIJUI ILA NILITEMBEA KWA MGUU KUJA KUKUZIKA


Aljumaa kareem 🖤

Baada ya Mahakama kutoa hukumu ya kifungo cha miaka miwili jela kwa kosa la kuua bila kukusudia kwa mwigizaji wa Bongo movie Elizabeth Michael (Lulu) mastaa mbali mbali wametokea kuguswa na tukio hili kwa kupost ktk kurasa zao za mitandao ya kijamii huku wengine wakikumbushia na kifo cha marehemu Steven kanumba.

Kupitia ukurasa wa Instagram mchekeshaji Idris Sultan yeye ameandika haya:
Najua ulikua hunijui ila nilitembea kwa miguu kutoka mbezi kimara mpaka kinondoni kuja kukuzika. Ni mda mrefu sana umekua ukitembea na...
sisi kuomba upumzishwe, sasa naamini utapumzika kabisa. Allah akufanyie wepesi na milele utabaki mioyoni mwetu. Tulifunga njia, kazi na hata kuhema vizuri wengine tulishindwa na tukapata depression kubwa sanaaaa yote kwasababu ulitugusa katika mfano usioelezeka. Naamini haki yako sasa imepatikana na namuombea sana mama yako apewe nguvu na amani ya moyo. Finally Rested.
Ni mimi wako katika matumaini ya urithi wa ufalme wa movie Tanzania, Idris Sultan

0 comments:

Post a Comment