Pages

Subscribe:

Saturday, November 4, 2017

MSAMI ATOA NENO NDOA YA UWOYA NA DOGO JANJA


Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, mwenye uwezo mkubwa wa kucheza hasa katika matumbuizo yake jukwaani, Msami Baby ambaye alishaingia katika orodha ya waliotoka kimapenzi na muigizaji ‘Irene Uwoya’, Bila kinyongo ametoa salamu za kheri na kutoa pongezi kuelekea ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya.

Ikidhaniwa kuwa ndoa ya msanii na staa wa ngoma ya ‘Nganenaro’ Dogo Janja na Muigizaji Irene Uwoya ingekutana na vikwazo kutokana na maoni ya baadhi ya mashabiki na wadau tofauti, Msami ametaka...
maisha marefu ya ndoa hiyo huku akazia msemo wa ‘Age is Just a Number’ katika kuweka hali ya hewa sawa kwa wale walioleteleza vikwazo kwa kigezo cha kutofautiana kwa umri wao.

Msami ameandika:  Ndoa ni jambo la kheri sana, pongezi kwako @dogojanjatz na @ireneuwoya8 mmefanya watu wajue umri ni number tu #ukubwawapuasiowingiWakamasi

Hata hivyo Dogo Janja na Irene mpaka sasa imethibitika kuwa ni mke na mme(Wanandoa) kwakuwa hisia za kila kinachoandikwa mitandaoni hasa kupitia akaunti zao rasmi za Instagram imethibitika kuwa lipo penzi zito kati yao na wamekubaliana kuchukua maamuzi hayo ya kuishi pamoja pasipo na dalili za kulazimishwa.

0 comments:

Post a Comment