Pages

Subscribe:

Thursday, November 9, 2017

NANDY: RAY C ALINIDHALILISHA ALIPO NISHAMBULIA MTANDAONI


Nandy amesema kitendo cha Ray C kumshambulia mtandaoni kwa kuimba wimbo wake, kilimdhalilisha. Amesema Ray C ni muimbaji aliyekuwa akimuangalia tangu akiwa mdogo na hivyo kumshambulia mtandaoni ni kitu kilichomuumiza. 

Wiki kadhaa zilizopita, Ray C alimshambulia Nandy kwa kuimba wimbo alioshirikishwa na Mez B, Kama Vipi kwenye Fiesta. Ameiambia Dizzim Online kuwa ukaribu wa Ray C na THT ambao wanamsimamia Nandy pia ulimfanya ashangazwe na...
mrejesho wa msanii huyo mkongwe.

Amedai kuwa licha ya kuandika kwenye Instagram kumwelesha Ray C kwanini aliimba wimbo wake na kumweleza anavyomheshimu, alimtumia ujumbe binafsi wa simu lakini hakujibiwa. “Sio kitu kizuri ni kama amenidhalilisha bila kosa,” amesema Nandy.

0 comments:

Post a Comment