Pages

Subscribe:

Thursday, November 9, 2017

OTILE BROWN: SIKUJUA KAMA TATTOO YA TATIANA NA YA RIHANNA ZINAFANANA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Kenya, Jack Juma Bunda a.k.a Otile Brown ameruka mita mia juu ya yeye kufahamu chochote kuhusu kuonekana kwa makusudi na kufanana kwa mchoro wa tattoo ya mrembo ‘Tatiana’ aliyetumika katika video ya wimbo wake mpya ‘Mapenzi Hisia’.

Akipiga stori, Otile Brown amesema kuwa hakufahamu kuwa tattoo ile inayoonekana chini ya kifua cha video queen Tatiana ilishapata umaarufu kwa...
kuchorwa na mrembo muimbaji kutoka Marekani, Robyn Rihanna Fenty a.k.a Rihanna.
Tattoo ya Rihanna inayofanana na Marembo Tatiana

“Tatiana ni a Super Model kutoka nchini Kenya na ni mwanabiashara, Nilipokuwa nafanya video ya mapenzi hisia sio kwamba nilikuwa na nia ya kupata mtu mwenye tattoo kama hiyo, maana sikujua kama amechora tattoo kama hiyo ya Rihanna.

Sasa hivi ndo nimegundua baada ya wewe kuniuliza ndo nikagundua Ahaa! kweli kumbe zinafanana. Ilitokea tu, nilimtaka yeye kwenye video na ilipofika wakati wa scene ya swimming pool na vitu kama hivyo ndo nikapata kuiona hiyo Tattoo. Nilikuwa sijui ila sasa najua” Amesema Otile Brown.

Hata hivyo video ya wimbo huo wa ‘Mapenzi Hisia’ umeongozwa na Director X Antonio na inawezekana alipenda tattoo hiyo itumike kupamba video kwakuwa aliionesha katika sura ya kuweka kuwa rahisi kubaki katika vichwa vya watazamaji watako bahatika kuiona video hiyo.

0 comments:

Post a Comment