Pages

Subscribe:

Monday, November 13, 2017

SIMBA WAANZA KUMSAKA MTOTO ALIYE VAA FULANA YENYE JINA LA MANULA

Klabu ya soka ya Simba inamtafuta mtoto ambaye picha yake inasambaa mitandaoni akiwa amevaa  fulana iliyoandikwa jina la golikipa namba moja wa klabu hiyo Aishi Manula.  

Taarifa ya klabu hiyo jana ambayo ilitolewa kwenye ukurusa maalum wa klabu kwenye mtandao wa Instagram imeeleza kuwa mtoto huyo anatafutwa ili waweze kulipa...
fadhila kwa mpenzi yake aliyoyaonesha kwa klabu na golikipa.

Klabu ya Simba imekuwa na utaratibu wa kuwafikia watu wenye kwenda mbali zaidi katika kuonesha mapenzi na ushabiki wao kwa wachezaji na kikosi kizima cha Simba.

Msimu uliopita wa 2016/17 Simba ilimtafuta kijana Aziz wa mkoani Dodoma baada ya kuonesha mapenzi yake kwa mshambuliaji Ibrahim Ajib ambaye alikuwa akichezea timu hiyo kabla ya kuhamia Yanga msimu huu.

0 comments:

Post a Comment