Wednesday, February 14, 2018
LINAH NA RECHO WAKANUSHA KUMCOPY VANESSA MDEE
Ikiwa ni siku chache zimepita tangu Linah na Rachel watoe ngoma yao mpya ‘Same Boy’, wamekanusha ngoma hiyo kukopi idea kutoka kwenye ngoma ya Vanessa Mdee na Maua Sama ‘Bounce’.
Linah ameiambia The Playlist ya Times Fm kuwa ngoma yao ina idea tofauti na ile ya kina Vanessa na isitoshe ngoma hiyo ilikuwepo...
kabla Bounce haijatoka.
“Hii yetu tunazungumzia ile kwamba kwa pamoja tunamtaka mwanaume mmoja lakini ile yao inaelezea wapo na huyo mwanaume lakini hawajuani, sisi ni watu ambao tunajuana,” amesema Linah.
Same Boy ni ngoma ya pili kwa Linah na Rachel kukutana katika ngoma moja baada ya kushirikishwa na kundi la Makomando katika ngoma yao inayokwenda kwa jina la Chap Chap.
Labels:
HABARI & UDAKU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment