Wawili hao wameanza kujitetea katika Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Mbeya kuhusu kosa wanalotuhumiwa la kutoa...
lugha ya fedheha kwa Rais Magufuli.
Akitoa utetezi wake mshtakiwa wa kwanza Joseph Mbilinyi ‘SUGU‘ amekana kutenda kosa analotuhumiwa nalo pamoja na kukosoa mwenendo wa kesi inayomkabili tangu kukamatwa hadi kufikishwa Mahakamani huku akikana sauti iloyochezwa Mahakamani inayodaiwa kurekodiwa kwenye mkutano wake mwishoni mwa mwaka 2017 akisema sio yake.
Mbunge huyo kupitia Mawakili wake wawili akiwemo Peter Kibatala amesema baada ya mkutano wake December 31, 2017 alipigiwa simu na RCO siku inayofuata akimuomba afike ofisini kwake kujadili mambo fulani ambayo hakuyaweka bayana.
Akijibu maswali ya upande wa utetezi ukiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali Mkoa wa Mbeya Joseph Pande Mbunge huyo amesema alipoitwa na RCO aliambiwa kuwa wanashinikizwa na wakubwa ikiwemo ngazi ya Mkoa na kutoka Makao Makuu kwamba wamkamate bila kutaja kosa lolote jambo analodai kushangazwa nalo.
Wakati huohuo mshtakiwa wa pili Emmanuel Masonga naye amekana kutenda kosa akieleza kutowahi kutoa lugha yoyote ya matusi wala fedheha dhidi ya Rais Magufuli na kwamba yeye siku ya mkutano hakuwepo bali alitoka ofisini kwake saa saba mchana ili kumpeleka mkewe hospitali.
Katika kusikiliza kesi hiyo Mbunge wa jimbo la Mikumi mkoani Morogoro amefika kushuhudia usikilizwaji shauri hilo.
Kesi hiyo ya jinai namba 12 ya mwaka 2018 imeahirishwa hadi February 9, 2018 wakati washtakiwa wataleta mashahidi wao na vielelezo vyao Mahakamani hapo kwaajili ya upande wa utetez kuwasilisha ushahidi wao unaotarajia kuwa na mashahidi wanane washtakiwa wamerudishwa rumande.
0 comments:
Post a Comment