Usiku wa Ulaya umeendelea usiku wa kuamkia leo kwa kukamilisha mechi 16 za ufunguzi wa hatua ya makundi.
Mabingwa
watetezi Real Madrid wakiwa nyumbani Santiago Bernabeu wameibuka na
ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Apoel. Mabao mawili kati ya hayo
yakifungwa na Cristiano Ronaldo na kumfanya kuwa mchezaji mwenye...
mabao
mengi zaidi katika UEFA pekee akiwa na mabao 107.
Liverpool wakiwa nyumbani wamelazimishwa
sare ya 2-2 na wababe wao wa fainali ya EUROPA 2016 Sevilla. Huku
Manchester City chini ya kocha mshindi wa UEFA mara mbili Pep Guardiola
wakiiadhibu Fayenood ya Uholanzi mabao 4-0.
John Stone mlinzi wa kati wa Manchester
City amejiwekea rekodi ya kuwa mlinzi wa kwanza kufunga mabao mawili
sawa na Lionel Messi na Ronaldo katika hatua ya makundi Tottenham wakiwa
Wembley wamelipiza kisasi kwa Borrusia Dortmund baada ya kuwachapa 3-1
Wajerumani hao.
Gabriel Jesus wa Man City ameungana na Romelo Lukaku kwenye orodha ya wachezaji waliofunga katika mchezo wao wa kwanza wa UEFA.



Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment