Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini Burundi ametekwa nyara katika mji
mkuu wa nchi hiyo na watu wenye silaha wakiwa wamevalia sare za jeshi
la polisi, kwa mujibu wa familia yake.
Leopold Habarugira mwenye umri wa miaka 54, ndiye mweka hazina wa chama cha upinzani cha...
Union for Peace and Development (UPD), na miongoni mwa wanachama wachache wa upinzani waliobakia katika taifa hilo tangu lilipotumbukia katika mgogoro mwaka 2015.
Mke wake wake, Liberates Nzitonda, ameliambia shirika la habari la Ujerumani (dpa) kwamba yeye na mume wake walikuwa wanafanya mazoezi na ghafla wakaona gari linakuja upande wao, likiwa na watu watatu wenye silaha na wakiwa wamevalia sare za polisi, ambao walimchukuwa mume wake na kumlazimisha kuingia kwenye gari lao.
Lakini msemaji wa jeshi la polisi Pierre Nkurikiye, amesema mamlaka hazina taarifa kuhusu utekaji huo.

Follow on Instagram
0 comments:
Post a Comment