Pages

Subscribe:

Monday, November 6, 2017

SHAMSA FORD: LAITI NINGESOMA NINGEKUWA MUIGIZAJI WA KIMATAIFA

Msanii wa filamu nchini Shamsa Ford amewaponda baadhi ya wasanii wa Bongo movie na kusema ukosefu wa elimu kati yao chanzo kikubwa tasnia hiyo kushindwa kuendelea na kupiga hatua kubwa na kudai wamekalia umbea, chuki, ushirikina na roho mbaya.  

Shamsa Ford amesema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram na kudai kuwa anatamani muda ungekuwa unarudi nyuma ili aweze kubadili maamuzi yake na kuweza...
kusoma ili kupata maarifa zaidi kwani anaamini wasanii wengi wa filamu nchini wanashindwa kusonga kwenda Kimataifa kwa kukosa elimu.

"Mama yangu alinikazania sana nisome kwa bidii wakati nipo shule ila nilipomaliza form 6 nikaona inatosha. COUNTER BOOK la shule nikaona zito ila SCRIPT ya movie nikaona jepesi..Natamani ningerudisha siku nyuma ningesoma kwa bidii hata kama ningetaka kuwa muigizaji basi ningekuwa muigizaji wa kimataifa mwenye maarifa. 


Moja ya vitu vikubwa vinavyoturudisha nyuma bongo movie ni elimu. Mtu aliyesoma na asiyesoma ni vitu viwili tofauti. sasa sisi wenge wetu hatuna elimu kabisaa" aliandika Shamsa Ford 

aliendelea kusisitiza kuwa "wengi wao darasa 7,5,2,6 wengine ndiyo kabisaa alijifunza kusoma na kuandika tu. Nakumbuka mwaka juzi nilimuona msanii wa Nigeria Genevieve akiojiwa CNN nikatamani niwe mimi. 

Wenzetu wamesoma ndiyomaana wametupita vitu vingi sana. Huku bongo movie kumejaa umbea, chuki, roho mbaya, ushirikina, mtu hata kama hujawahi kumkosea lakini akikaa na watu wanaokuchukia atakusema vibaya, Lakini pia ukijitenga useme uishi kivyako utaambiwa unalinga na vikao utaekewa. Yote haya ni kwasababu ya ukosefu wa elimu ndomaana watu wanaweza kupoteza muda kwa vitu vya kijinga" alisisitiza Shamsa Ford

0 comments:

Post a Comment