Pages

Subscribe:

Wednesday, February 7, 2018

MIMI MARS: JUX NI MTU POA NA NIZAIDI YA SHEMEJI KWANGU


Msanii wa kike anayefanya vizuri kwenye mziki wa Bongo fleva Mimi Mars ambaye jina 
lake halisi ni Marianne Mede amefunguka na kudai kuwa shemeji yake msanii wa Bongo 
fleva ni zaidi ya shemeji tu kwake.
 
Mimi Mars ambaye ni mdogo wa msanii supastaa wa Bongo fleva nchini Vanessa Mdee
amekuwa akitoa ngoma ambazo zimekuwa zikikubalika sana na kufanya vizuri mfano 
kama vile ''Dede'' , shuga na... wimbo wake mpya aliouachia hivi karibuni unaoenda kwa 
jina la ''Sitamani''. 
 
Mimi Mars alifanya mahojiano na Global Publishers ambapo alifunguka mengi kuhusu 
muziki wake mipango yake ya kuachia albamu lakini pia ameongelea mahusiano ya dada 
yake Vanessa na mpenzi wake Jux.
 
Nina mpango wa kuachia albamu mwakani lakini kwa sasa nataka mashabiki wangu 
waifahamu kwanza sauti yangu na nguvu yangu ya kimuziki ili nitakapotoa albamu 
waweze kufurahia zaidi lakini pia napenda kuwaambia mashabiki zangu kuwa 
nimechaguliwa kuwania tuzo Ami Africa Awards hivyo naomba mashabiki 
zangu wanipigie kura ili tulete tuzo nyumbani. 
 
Lakini pia Mimi Mars amefunguka juu ya uhusiano wa dada yake Vanessa na mpenzi 
wake Jux: Jux ni mtu poa kusema ukweli ninaweza kusema ni zaidi ya shemeji kwangu 
anajali na ana upendo wa Shari, ana upendo na ana heshima na ninamshukuru kwa 
anavyompenda dada yangu na ninaona anamfanya kuwa mtu bora katika kazi zake na 
hata maisha yao ya kawaida.

0 comments:

Post a Comment