Mbunge wa Australia George Robert Christensen amejikuta akikabiliwa na
wakati mgumu pamoja na shutuma baada ya kutuma picha kwenye ukurasa wake
wa Facebook akiwa na bastola huku akidaiwa kutoa maneno ya kejeli kwa
wafuasi wa Chama cha Green.
Maneno yanayodaiwa kuambatanishwa na picha hiyo yamesomeka "mnahisi mna bahati,ninyi watu msio na...
thamani" (“Do you feel lucky, greenie punks?”)
Chama cha Green kimesema kwamba kauli iliyotolewa na mbunge huyo wa Chama cha Conservative ni ya kusikitisha sana na kuainisha kwamba ameitoa kipindi ambacho watu 17 wameuwawa nchini Marekani katika shambulio la bunduki katika shule moja jimboni Florida..
Polisi katika mji huo imesema kwamba inaangalia uwezekano wa ikiwa uchunguzi unaweza kufanyika au la ingawa mbunge huyo amekaririwa akisema kwamba kauli hiyo aliyoituma ilikuwa utani.
Waziri Mkuu wa nchi hiyo Malcolm Turnbull amesema kauli hiyo iliyotumwa katika ukurasa wa facebook wa mbunge huyo haikuwa sahihi.
Taarifa nyingine kutoka makao makuu ya jeshi la polisi nchini humo imesema inapima kauli hiyo kabla ya kuchukua hatuahuku Wapinzani wa kisiasa wakimshutumu Christensen kwa kuchochea vurugu.

0 comments:
Post a Comment