Pages

Subscribe:

Monday, October 31, 2016

HII NDIYO TAARIFA YA KIFO CHA BONDIA THOMAS MASHALI

post-feature-image
Bondia Thomas Mashali ameuawa usiku wa kuamkia leo kwa kupigwa na watu baada ya kudaiwa kuitiwa kelele za mwizi, kwa mujibu wa taarifa ya mtu wake wa karibu.

Mashali aliyezaliwa kwa jina Christopher Fabian Mashale aliuawa baada ya kupigwa akiwa huko Kimara jijini Dar es Salaam. Inasemekana wakati akinywa pombe, ulizuka ugomvi na mtu mmoja ambaye...

anadaiwa kupiga kelele kusema Mashali ni mwizi na watu kuanza kumshambulia.

Ndugu zake wanadai kuwa walimkuta akivuja damu nyingi.

Taarifa zinadai kuwa alipelekwa katika hospitali ya Sinza Palestina kabla ya kupelekwa Muhimbili ambako mauti ilimkuta. Inasemekana kuwa hadi jioni alikuwa na bondia mwenzake, Francis Cheka.

0 comments:

Post a Comment