Pages

Subscribe:

Monday, October 31, 2016

KALA JEREMIAH: WANANDOTO RMX WASHIRIKI 8 WAMESHA INGIZA VOCAL


Takriban miezi miwili sasa imepita tangu msanii wa Hiphop Kala Jeremiah alipotoa ahadi ya kufanya remix ya wimbo wake wa “Wanandoto” na mashabiki zake wenye vipaji na kutoa tamko la kwamba mashabiki hao wawe wanajirekodi video fupi huku wakiimbia beat ya Wanandoto kwa kutumia mistari yao binafsi na kupost katika kurasa zao za instagram na kuweka hash tag ya Wanandoto (#Wanandoto).

Ukimya umetawala juu ya suala hilo, ndio sababu zilizofanya mwandishi kupiga story na mkali huyo na kutaka kujua uliishia wapi mchongo huo.
“Project ya wanandoto remix inaenda vizuri na...
washiriki wote 8 wamekwisha ingiza sauti, kutoka mikoa mbali mbali na mmoja kutoka Kenya. Imebaki tu sehemu yangu mimi kwasababu nina kama miezi miwili sipo Dar, niko mikoani kuna kazi fulani naifanya na hivyo mimi ndio nimekuwa kama kikwazo katika ucheleweshwaji wa hii project. Lakini all & all mwishoni mwa mwezi wa 11 narudi Dar es Salaam na kitu cha kwanza ni kwenda studio na kukamilisha hicho kitu na baada ya hapo process zingine zitafuata.”
Hayo ndio yalikuwa majibu ya Kala Jeremiah

0 comments:

Post a Comment