Pages

Subscribe:

Friday, October 28, 2016

ALI KIBA: WALIOSHINDA TUZO ZA MTV MAMA WALISTAHILI USHINDI


alikiba
Mkali wa wimbo ‘Aje’ AliKiba amefunguka na kuzungumzia ushiriki wa watanzania kwenye tuzo za MTV Mama Awards 2016. Muimbaji huyo ambaye alikuwa miongoni kati ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tuzo hizo na pia aliwania tuzo ya ‘Best Collaboration’ ya wimbo wa Unconditionally Bae alioshirikiana na Sauti Sol, amesema watanzania walijitahidi lakini walizidiwa na wasanii wa nje ndiyo maana wakashindwa kutamba.

“Katika ushindani kuna kushinda na kushindwa sisi hatusemi kuwa tumeshindwa na naamini Tanzania ina vipaji sana na kila msanii anajitahidi kufanya kwa uwezo wake ili...
aweze kufikisha nchi yetu sehemu nzuri,” AliKiba alikiambia kipindi cha Clouds 360. “Kwasasa muziki wetu umekuwa kwa kasi sana na unazidi kutanuka.

 Kwa washindi ambao wameshinda kwenye tuzo za ‘MTV Mama Awards’ wanastaili kwasababu kazi wamefanya na tumeziona”
Katika hatua nyingine muimbaji huyo amewataka mashabiki wa muziki wake kukaa makao wa kula kwa ajili ya ujio wa kolabo yake mpya yakimataifa.

0 comments:

Post a Comment