Pages

Subscribe:

Tuesday, October 25, 2016

DOGO JANJA NA YOUNG KILLER WAZIDI KUPIGANA VIJEMBE


 
Tumezoea kuona wasanii wakitafuta kiki kwa njia tofauti tofauti kwa sasa lakini hii imeonekana kuwa siyo kiki bali ni ukweli mtupu. Young killer na Dogo janja wamepigana vijembe huku kila mmoja akijitamba kuwa yeye ni mkubwa kuliko mwenzake. 
 
Mwandishi alimtafuta Dogo Janja na kuzungumza naye na alisema kuwa hajaona msanii wa kushindana nae kwa sababu yeye ndiye 'role model' wa madogo wote walioimba muziki hata Young Killer yeye ndiye...
aliyemshawishi aingie kwenye muziki kwa hiyo "huwezi fananisha Port na Bugati"

“Mimi siokoi rap naokoa maisha wao waache waendelee mimi huwezi nifananisha na yule. Dogo Janja anayechana ni mmoja tu na mimi na huyo Young Killer mimi ndiyo niliyemuinspire kenye muziki kwa hiyo muache aongee tu, kingine huwezi fananisha port na bugati.” amesema Dogo Janja.


Pia mwandishi alimtafuta Young Killer na kuzungumza naye alisema kuwa haoni kama dogo janja anaimba rap bali anaimba miziki yao ya kibiashara na yeye ngoma yake ya mwisho aliyofanya na Mr. Blue ndiyo aliyofanya rap kweli. Pia aliongezea kwa kusema kuwa  yeye ndiyo mkali kuliko wote.

“Dogo Janja siyo rapa mimi ndiyo rapa mkali kuliko wote, Dogo Janja anaimba muziki wa biashara ila mimi naimba rap ya kweli ukisikiliza ngoma niliyofanya na Mr. Blue utanielewa kwa hiyo mimi ni mkali kuliko Dogo Janja|”
Hata hivyo sisi tumewaachia mashabiki waseme wanaonaje kwa mtazamo wao kuhusu mtanange huo.

0 comments:

Post a Comment