Pages

Subscribe:

Friday, October 28, 2016

KAJIANDAE YA OMMY DIMPOZ NA ALIKIBA KUTOKA SOON


Amefunguka kupitia kipindi cha Clouds 360 cha Clouds TV mfalme wa Bongo Fleva Alikiba kuhusiana na ujio wa ngoma mpya ambayo kashirikishwa na Omary Nyembo almaarufu kama Ommy Dimpoz.


kama unakumbuka vizuri ngoma ya “Nai Nai” ndio ngoma ambayo ilimtambulisha Ommy Dimpoz katika game ya music, kutokana na ukali wa ngoma hiyo na mapokezi ikiwa ngoma hiyo...
Ommy alifanya na Alikiba.

Kuna kila sababu ya ngoma hiyo ya “Kajiandae” kuwa kali kutokana na ufanyaji wa kazi nzuri wa wasanii hao na pia King Kiba amelithibitisha hilo kwa kuongea haya.

“Wimbo ni mkali, na hata maandalizi ya video tumekwisha fanya cha msingi ni mashabiki wangu na mashabiki wa Ommy kukaa mkao wa kula wakati wowote watapokea ladha nzuri kwasababu najua ni kitu gani wao wanataka.”

0 comments:

Post a Comment