Pages

Subscribe:

Thursday, October 27, 2016

DYNA NYANGE: NITAFANYA KAZI NA LEBO ITAKAYO KUBALI MASHARTI YANGU


dayna-nyange
Dayna Nyange amefunguka kuwa atakuwa tayari kuwa chini ya lebo yoyote endapo watakubaliana na masharti yake. Hitmaker huyo wa ‘Komela’ amemuambia mtangazaji wa Maisha FM ya Dodoma, Silver Touchez “Kikubwa nachoangalia ni sababu, kabla sijajiunga na lebo yoyote lazima niwe na vitu vyangu ambavyo navitaka na wao wanavitu vyao wanavyotaka.”

“Record label ni studio tu ambao watu watakuwa wanasimamia kazi zangu ni kitu ambacho mimi mwenyewe ninaweza nikaenda...
sehemu yoyote nikafanya kazi zangu. Kuna vitu vingi sana kabla hujaingia kwenye lebo yoyote kama kuna makubaliano mazuri yatakuwepo basi tutafanya kazi,” ameongeza. 

Katika hatua nyingine muimbaji huyo amekanusha kuwa hana mahusiano ya kimapenzi na Idris Sultan zaidi ya kuwa marafiki tu.

0 comments:

Post a Comment