Pages

Subscribe:

Tuesday, October 25, 2016

JOH MAKINI: AKINA DADA RUKSA KUJIUNGA WEUSI

Rapa Joh Makini ambaye anafanya vyema na wimbo wake wa 'Perfect Combo' amefunguka na kusema kuwa milango iko wazi kwa wasanii wa kike kujiunga na kundi la Weusi na kufanya nao kazi. 

Joh Makini amesema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ambacho kilikuwa kinaruka moja kwa moja kutokea Kituo cha Mabasi cha Sinza Jijini Dar es Salaam 'Simu 2000' ambapo...
moja ya shabiki wa kike aliomba nafasi kujiunga na kundi hilo pindi atakapo maliza shule.

"Milango iko wazi kwa wadada kuja kuungana nasi, na tuombe Mungu kwani muda si mrefu tunampango wa kuja la 'Label' ya Weusi ambayo itatoa nafasi kwa wasanii mbalimbali" alisema Joh Makini 

Mbali na hilo Joh Makini alifafanua kuwa toka ameanza muziki hajawahi kuwa na tofauti na mwanamuziki yeyote yule kwani yeye hafikiri kuwa na tofauti na msanii mwingine kama itamuongezea kitu

"Toka nimeanza muziki sijawahi kuwa na bifu na mtu yoyote, sijawahi kufikiri kuwa na tofauti na mtu inaweza kuniongezea kitu, mimi na 'deal' na muziki wangu" alisema Joh Makini

0 comments:

Post a Comment