Pages

Subscribe:

Thursday, October 20, 2016

BEKA IBROZAMA KUJA NA BENDI YA SPIDOCH

Beka Ibrozama
Msanii wa muziki, Beka Ibrozama amesema maandalizi ya bendi yake mpya iitwayo ‘Spidoch Band’ yamekamilika ambapo kwa kwa sasa anajipanga kuachia wimbo wa bendi hiyo pamoja na kufanya uzinduzi. Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na video ya wimbo ‘Mwanza’ ameiambia Bongo5 kuwa hana muda zaidi wa kuwachelewesha tena mashibiki wake ambao tayari alishaisubiria bendi hiyo kwa muda mrefu.

“Bendi imekamilika kabisa, jina la bendi ni ‘Spidoch Band’ na hivi karibuni nitaachia wimbo wa bendi yangu na baada ya hapo ndo...
nitafanya uzinduzi wa bendi rasmi lakini kwa ufupi bendi imekamilika kabisa,” alisema Beka.
Muimbaji huyo amesema amechukua muda mrefu kuiandaa bendi hiyo ili kukabiliana na ushindani uliyopo kwenye muziki wa bendi.

0 comments:

Post a Comment