Pages

Subscribe:

Tuesday, October 25, 2016

MALAIKA: MWANAUME LIJARI HAWEZI KUISHI KWA MWANAMKE

 
Msanii wa muziki wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa anafanya vizuri wa wimbo wake wa 'Rarua' Malaika amefunguka na kusema kuwa hakuna mwanaume lijali na mwanaume aliyekamilika ambaye anaweza kuishi kwenye nyumba ya mwanamke. 

Malaika alisema hayo alipokuwa akionesha hatua iliyofikia nyumba yake hiyo na kudai kuwa haamini kama kuna mwanaume atakuwa tayari kuja kukaa kwenye nyumba ambayo yeye amejenga kwa jasho lake, Malaika anadai nyumba hiyo...
ameweza kuijenga kwa pesa za muziki na dili nyingine mbalimbali hivyo alianza mdogo mdogo mpaka sasa anakaribia kuhamia.

"Sidhani kama kuna mwanaume lijali, mwaume kamili ambaye anaweza kuishi kwenye nyumba ya mwanaume, au nyumba aliyojenga mwanamke, dunia ya leo ukiona mwanamke ana gari zuri, nyumba nzuri lazima hapo mwanaume ujipange. Hivyo sidhani kama mwanaume atatoka mwanaume huko aliko na kuja kuishi kwangu" alisema Malaika 

malaika-2
Hitmaker huyo ‘Zogo’ amekiambia kipindi cha Ujenzi cha East Africa TV kuwa nyumba hiyo imemgharimu kiasi cha shilingi milioni 30 mpaka sasa ilipofikia ambapo kwa zaidi ya asilimia 90 imeshakamilika. Hizo ni gharama nje ya kiwanja.

Malaika ameongeza kuwa familia yake ndiyo iliyochangia yeye kujenga nyumba hiyo kwa kuwa walimshauri mapema kufanya hivyo kabla hajaachana na mpenzi wale ambaye pia alikuwa akimsimamia kazi zake za muziki.

Alisema kuwa hakuamini kwa kidogo alichokuwa anapata angeweza kujenga nyumba yake na ikakamilika. Kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na wimbo wake ‘Rarua’ uliotoka April, mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment