Pages

Subscribe:

Thursday, October 20, 2016

DULLY SYKES KUJA NA TOUR YA DAR

dully-sykes
Msanii wa muziki anayefanya vizuri na wimbo ‘Inde’ Prince Dully Sykes amejipanga kuja kivingine katika tour yake jijini Dar es salaam ambayo itaanza weekend hii Club 71. Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Dully amesema ameamua kufanya baadhi ya mabadiliko kwenye team yake ili kuonyesha utofauti wa Dully wazamani na huyu wa sasa.

“Mikoani mambo yalikuwa mazuri sana namshukuru Mungu na sasa ni zamu ya Dar es salaam,” alisema Dully “Tour yangu ya Dar itaanzia Club 71. Kutakuwa na...
surprise zakutosha, pia Dully nitakuja kivingine nikiwana na mabaunsa, kwa sababu huyu pia ni Dully mpya ambaye anahitaji usalama kwenye show zake,”
Muimbaji huyo amesema katika show hiyo atasindikizwa na wasanii ambao atawaweka wazi hapo baadae.

0 comments:

Post a Comment