Pages

Subscribe:

Friday, October 28, 2016

Z ANTO: UKIWA NA SIX PACKS UNATOKA KIMUZIKI


 
Msanii Z Anto ambaye amewahi kutamba kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva amefunguka na kusema muziki wa bongo fleva sasa hivi ni rahisi sana kwani msanii akiwa na 'Six Pack' harafu akaimba imba tu anatoka kimuziki tofauti na zamani.  

Z Anto alisema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio hivi karibuni alipokuwa kwenye heshima ya bongo fleva na kusema hiyo kwake si changamoto yeye...
kurudi kwenye muziki kwani anatambua ana uwezo wa juu na anaweza kufanya jambo kubwa sababu aliwahi kutamba kipindi ambacho msanii kutamba lazima awe amefanya kazi kweli na si kukurupuka tu.

"Muziki wa bongo fleva wa sasa mwepesi sana zamani kulikuwa na mazingira magumu na uchache wa watayarishaji hivyo kupata nafasi lazima uwe msanii kweli na una uwezo wa hali ya juu, zamani ili uimbe na usikike ilikuwa lazima ufanye kazi kweli kweli lakini saizi muziki mwepesi sana maana ukiwa na 'Six Pack' tu kisha ukaimba imba eti unatoka" alisema Z Anto 

Mbali na hilo Z Anto aliweka wazi kuwa ana mpango wa kurudi kwenye muziki na kufanya kazi kweli kweli hivyo yupo kwenye mchakato wa kuona anafanya kazi na 'Label' gani ambayo inaweza kumpeleka sehemu ambayo yeye anataka kufika kimuziki.

0 comments:

Post a Comment