Rapa Nay wa Mitego ambaye anafanya vyema na wimbo wake 'Sijiwezi'
amefunguka na kusema kuwa ni kweli alikuwa amezinguana na mama yake
mzazi na walikaa miaka mitano bila kupiga stori yoyote ile.
Nay
wa Mitego alisema haya kupitia kipindi cha Planet bongo na kusema kwa
sasa wameshamaliza tofauti zao na anaishi na mama yake mzazi ingawa
anakiri kuwa ni kweli ameishi... zaidi ya miaka mitano bila kuongea na mama
yake mzazi.
"Mimi na mama mzazi tuko poa sana na nina kaa naye this time, ni
kweli kabisa tumekaa miaka mitano bila kuzungumza jambo lolote lile ila
ni mazingira ya maisha ya mtaa niliyokuwa naishi lakini mpka muda huu
tunaongea mimi naishi na mama yangu nyumbani kwangu, hivyo niko naye
nyumbani" alisema Nay wa Mitego
Mbali na hilo Nay wa Mitego anasema yeye haamini katika dini kwani
anaona dini nyingi saizi zimekuwa biashara, hivyo yeye anamini Mungu na
anajua Mungu yuko kila sehemu si lazima iwe kanisani.
0 comments:
Post a Comment