Pages

Subscribe:

Friday, January 20, 2017

BILLNAS: WIMBO WANGU MPYA 'MAZOEA' NILIUREKODI TANGU MWAKA 2014


Msanii wa muziki wa hip hop, Billnas amedai wimbo wake mpya ‘Mazoea’ aliyomshirikisha rapper Mwana FA aliurekodi toka mwaka 2014. Rapper huyo ambaye yupo chini la label ya LFLG, ameadi amekuwa na tabia ya kurekodi nyimbo nyingi na kuziweka kusubiria muda sahihi wa kuziachia.

“Nyimbo ya mazoea nilirekodi tangu mwaka 2014,” Billnas alikimbia kipindi cha Ubaoni cha EFM. “Unajua ukiwa na nyimbo nyingi ndani kuna utulivu fulani unakuja kwa msanii, kwa sababu tayari...
ndani una ngoma za kutosha ambazo zinasubiria muda wakutoka,”

Kuhusu wimbo wake wa ‘Mazoea’ rapper huyo amedai ameachia wimbo huo ili kuwataka watu kupunguza mazoea kwani mazoea hupunguza heshima.
“Mtu hawezi kutunza heshima kama akikuzoea sana,” alisema Billnass.

0 comments:

Post a Comment