Pages

Subscribe:

Friday, January 20, 2017

AIKA AZUNGUMZIA ISHU YA NAVY KENZO KUFANYA KAZI NA PAH ONE


Kama ulikuwa hauja sanuka acha nikusanue, kabla halija zaliwa kundi la Navy Kenzo lilikuwepo kundi la Pah One, kundi ambalo liliviunganisha vichwa kibao wakiwemo Nahreel na mwanadada Aika ambao leo wanaliunda kundi la Navy Kenzo kabla ya kutofautiana na washkaji zao wa Pah One.

Story nyingi zilisikika kuhusu mfarakano huo wa kundi la Pah One ikiwemo ma-beef na vitu kama hivyo hadi pale D’Weekend Chatshow ya Clouds TV ilipoamua kuwakutanisha wakali hao na...
kuweza kumaliza tofauti zao.

Pamoja na kumaliza tofauti, kila pande iliendelea kupiga mbishe zake kama kawiz, na ni ukweli usiofichika kuwa ni Navy Kenzo ndio ambao walipata mafanikio makubwa sana kwenye muziki zaidi ya Pah One.

Sasa moja kati ya vitu ambavyo vimetrend kinoma hapo jana ni pamoja na picha iliyosambaa mitandaoni ikiwaonyesha wakali wa Pah One wakiwa pamoja na Navy Kenzo.
Kitu ambacho kilizua maswali mengi kwa mashabikii na kuwapa hamu ya kutaka kujua kwamba kuna kazi ambayo inafuata ya pamoja ya wakali hao au ni vipi!
Perfect255 imepiga story na Aika wa Navy Kenzo na amefunguka kila kitu kuhusiana na kukutana kwao na Pah One na mengine mengi kuhusu kazi.

“Pah One waliomba mkutano na sisi na huu ndio mkutano wakwanza tumekutana nao, wameomba kurudi kwenye system ya music na kama unavyojua Nahreel ndio producer wao, ndio anawatambua kiundani zaidi jinsi ya kufanya nao kazi pamoja na quality ya muziki wanaoufanya Nahreel anaweza akaifanyia kazi ikawapeleka sehemu zaidi.”

0 comments:

Post a Comment