Pages

Subscribe:

Thursday, January 5, 2017

GK AIPA SERIKALI RAMANI YA KUWANASA WAUZA UNGA

Ikiwa sakata la madawa ya kulevya linazidi kuchukua sura mpya nchini kutokana na vijana wengi kuingia katika matumizi ya dawa hizo Rapa King Crazy GK kutoka East Coast Team ameitaka serikali kutowapuuzia watu ambao wanauza madawa ya kulevya.

Gk ametoa neno hilo kwa serikali na kusema kuwa watu hao ni hatari kwani wanauza sumu ambazo mwisho wake zinaua vijana ambao ni...
nguvu kazi ya taifa.

King Crazy GK ameitaka serikali isiwachekee hata kama ni watu maarufu au wanamuziki wanapaswa kupewa adhabu kali sana kwani hao ndiyo kioo cha jamii pia ametoa rai kwa vyombo vya usalama kuwashirikisha wananchi kwani wanajua ukweli juu ya sakata la madawa ya kulevya.

“Mtu anayebeba au kuuza unga ni kama mchawi, na nchi za watu wakikamatwa wananyongwa kwa sababu anauza sumu inayoua watu lakini kwetu hapa mtu anayeuza na kubeba madawa ya kulevya anaonekana ndiye mjanja. Inabidi serikali isiwachekee hawa watu hata kama ni wanamuziki inabidi wapewe adhabu kali sana sababu hao ndiyo kioo cha jamii, hivyo wanapoendelea kuchekewa wanalisha sumu kwa jamii na kuona hayo ndiyo maisha yenyewe watu wanapaswa kuishi kumbe siyo”. Alisema King Crazy GK

0 comments:

Post a Comment