Pages

Subscribe:

Thursday, January 5, 2017

BILLNAS: 2017 NTAACHIA NYIMBO NYINGI NAANZA MWEZI HUU


Hit maker wa wimbo ‘Chafu Pozi’ Billnas amefunguka na kueleza mipango yake mipya ndani ya mwaka 2017 baada ya kufanya vizuri mwaka uliyopita. Akiongea na Bongo5 Jumatano hii Billnas amedai mwaka huu ataachia ngoma nyingi zaidi kuliko mwaka uliopita.

“Kusema kweli mwaka 2016 ulikuwa wa mafanikio sana katika maisha yangu, ni mwaka ambao imefanya muziki, show nyingi, muziki wangu umepanuka zaidi,” alisema Billnas. “Mwaka 2017 kuna...
mengi yanakuja kutoka kwangu, kwanza huu mwaka nitakuwa na ngoma nyingi sana na mwezi huu nitaachia wimbo mmoja. Kwa hiyo mwaka huu naweza kusema nitaachia ngoma nyingi kuliko hata miaka iliyopita,” aliongeza.
 
Rapper huyo amedai hatawaangusha mashabiki wake kwani wamejipanga kuendeleza wimbi lake la kufanya vizuri.

0 comments:

Post a Comment