Pages

Subscribe:

Friday, January 20, 2017

CHALE 21 ZA DIAMOND PLATNUMZ ZAZUA GUMZO

dai1
Alama 21 zinazodaiwa ni chale zinazopatikana mgongoni mwa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ zimezua mambo baada ya juzikati picha yake kutupiwa mtandaoni ikizionesha kwa uwazi na kuibua mjadala mzito.

Picha hiyo iliyotupiwa mtandaoni ilimuonesha Diamond akiwa kwenye moja ya shoo alizofanya hivi karibuni huku akizungushiwa eneo ambalo lilionekana kuwa na chale, jambo lililowafanya... wadau kibao wazijadili.

Mmoja wa mashabiki hao aliandika hivi: “Duh! Huyu jamaa hakamatiki aisee, kwenye shoo zake ni nyomi, anang’ara kimataifa, utajiri wake usiseme, au ndiyo tuseme hizi chale zake alizochanjwa ndiyo sababu?

“Yaani kama ni hivyo na mimi aniambie tu kachanjwa wapi ili na mimi niende kwa huyo mganga wake.”
Mwingine akaandika hivi: “Acheni zenu, huyu Mond ana nyota yake tu, hizo chale inawezekana ilikuwa ni tiba ya kawaida.

Akizungumza  mmoja wa wasanii anayefanya poa licha ya nyota yake kutong’ara sana, D-Malick alisema:

“Unajua nasikia tu kwamba huwa wasanii wakubwa wanaendaga kwa wataalam ‘kutengenezwa’ ili washaini, niliona picha moja inaonesha Diamond akiwa amechanjwa chale mgongoni, aisee kama ndizo zinamfanya awe na mafanikio hayo makubwa ipo siku nitamfuata anielekeze na mimi niende.”

  jitihada za kumtafuta Diamond kuzungumzia mjadala huu ulioibuka kuhusiana na chale zake zikihusishwa na kung’ara kwake lakini hakuweza kupatikana mara moja.

Hata hivyo, siku za nyuma Diamond aliwahi kuongea  na kusema kwamba, madai kuwa kufanya kwake vizuri kwenye muziki kunatokana na mambo ya kishirikina siyo kweli bali juhudi binafsi ndizo zilizomfikisha mahali alipo.

“Mafanikio yangu hayatokani na mambo ya kishirikina, juhudi na maarifa ndiyo siri ya mafanikio yangu,” aliwahi kusema hivyo Diamond.

0 comments:

Post a Comment