Pages

Subscribe:

Friday, January 20, 2017

HII NDIYO MIANGO YA WCB KA MWAKA 2017


Baada ya kufanya vizuri na ngoma kibao ambazo zimeufanya muziki wa Bongo fleva kufikia levo za Kimataifa, Label ya WCB imeamua kuja na jambo jingine kubwa ambalo litafanya wigo wa muziki kutanuka zaidi bongo.

Kupitia kipindi cha XXL leo Alhamis tarehe 19 ambapo AY alikuwa pamoja na meneja wake Sallam kuzindua wimbo mpya wa ‘More and More’, Sallam Sk aliamua kufunguka mipango ya WCB kwa mwaka huu na kusema kwamba kikubwa ambacho wanakipanga kwa sasa WCB ni kusaini...
label zenye wasanii ambao label kama label wanaweza kutoa nyimbo na kuifanyia promotion alafu WCB wakaifanya distribution na Publishing  katika kazi za wasanii wengine, Ishu hiyo imekuja baada ya WCB kushare partner na Universal Music Group.

“Ebhana swala la Management sasa hivi limekuwa kabisa, tunatafuta wigo kabisa wakuwa na management nyingi kabisa hiyo cha kwanza na kama WCB tunaweza kuchukua wasanii ambao wapo kwenye label ya WCB lakini tumeona sasa tukichukua wasanii wengi unakuwa unawabana wasanii wengine kuchelewesha kutoa kazi zao, sasa tunachokifanya sasa hivi wigo ambao tunaenda kuutanua sasa hivi WCB as a WCB kwasababu inashare partner na Universal, kwahiyo sasa WCB inasaini logo…..kwahiyo sasa hivi tunachoangalia ni kusaini label ambazo zenye wasanii ambayo label kama label wao wanaweza kutoa nyimbo na kufanya promotion, sisi WCB tukafanya Distribution na publishing katika kazi zaokwahiyo tutaweza kupromote kazi zao, kwahiyo itasaidia wigo wa muziki kutanuka zaidi Tanzania na kulileta soko la Muziki Tanzania katika manufaa ya waTanzania nzima…plan ya mwaka 2017” Alisema Sallam SK

0 comments:

Post a Comment