Pages

Subscribe:

Thursday, January 5, 2017

HILI NDIYO JAMBO LILILO MFANYA Q-CHILLA KUACHANA NA UNGA

Msanii Q Chief amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa zilizopolekea yeye kuachana na matumizi ya dawa za kulevya na kusema yeye alipitia njia ngumu zaidi ya kuachana na matumizi ya dawa hizo kwa kupambana na nafsi yake.

Amesema hiyo ni tofauti na wasanii wengine ambao wamekuwa wakilazimishwa kuacha ili hali wao bado wanaupenda unga na hawapo tarayi kutoka moyoni mwao.
Q Chief alisema hayo alipokuwa akiongea na EATV na kusema jambo la kwanza kabisaa lilimfanya apigane...
vita na nafsi yake kwanza aliwatazama watoto wake wa kike watatu na kuona hawana furaha kuona baba yao yuko vile.

“Kiukweli mimi nilianza kupigana na nafsi yangu mwenyewe nilianza kujiaminisha kuwa hiki kitu si kizuri kwa afya yangu nataka kuacha, nikasema sasa basi, nina watoto watatu wa kike, mimi ni baba wananihitaji, nina fani yangu na nina mambo mengi ya kufanya”. Alisema Q Chief

0 comments:

Post a Comment