Pages

Subscribe:

Friday, January 6, 2017

GODZILLA: MWAKA 2017 NI KAZI JUU YA KAZI


12547500_1666850613574464_1906674967_n
Mwanamuziki wa Hip Hop bongo Golden Jacob, maarufu kwa jina la Godzilla ambaye siku ya jana ametimiza miaka kadhaa katika maisha yake. GodZilla amefunguka na kusema kuwa mwaka 2017 yeye ni kazi tu kwani atakuwa akiachia kazi baada ya kazi mpaka mwaka utakapokwisha.
 
Godzillah amedai kuwa tayari amejipanga kwa mwaka 2017 na ana kazi za kutosha huku akiwa amejipanga kuongeza vitu vipya zaidi katika muziki wake ambavyo vitaleta...
tija na hamasa katika muziki wa hip hop.

“Kwanza nashukuru Mungu kuongeza mwaka mwingine tena lakini mwaka 2017 kwangu mimi ni muziki baada ya muziki, na kuongeza vitu vipya zaidi, cha msingi tuombe uhai” alisema Godzilla ndani ya EATV

Mbali na hilo Godzillah alisisitiza kuwa kuanzia sasa muda wowote ule ataachia kazi yake ya kwanza ambayo ndiyo itakwenda kufungua mwaka 2017 katika muziki wake.

0 comments:

Post a Comment