Pages

Subscribe:

Friday, February 9, 2018

LULU DIVA: SIWEZI KULIA ETI KISA NIMEACHWA NA MWANAUME

Baada ya kusambaa kwa video mitandaoni ikimuonesha msanii Lulu Diva akilia kwa uchungu na kuhusishwa kuachwa na 'sponser' (mfadhili ) anayemuweka mjini, msanii huyo amesema kwamba hawezi kulia kwa kuachwa kwani hapungukiwi na chochote wala hatokuwa wa kwanza kufanyiwa hivyo.

Mbele ya kamera za eNewz Lulu amesema kwamba kilio chake hakihusiani kabisa na maswala ya mahusiano na wala hajaachwa na mpenzi wake bali alikuwa na mambo yake mwenyewe ambapo aliamua kulia ili...
kupunguza hasira na kujiweka sawa kwani hasira zake zinapungua pale anapolia.

Msanii huyo amesema kwamba yeye siyo malaika kwani kuna muda anapata maudhi na haijalishi kama ni ya kimapenzi au lakini pia ameongeza.

"mimi siwezi kulia eti kisa nimeachwa na mwanaume kwani hata nikiachika sipungukiwi chochote sana sana nitamuache aende zake nami nitaendelea na maisha yangu kwani sitokuwa wa kwanza kuachwa mimi.." .

Ameongeza "mtu kama anataka kuondoka anaondoka zake tu siwezi kumzuia kwani mimi nikizaliwa mwenyewe na habari za kusema nimepokonywa gari na huyo sijui ni danga si kweli kwani  mimi gari nilinunua kwa pesa yangu na mpaka saizi ndilo nalotumia watu wasizushe maneno.. ".

0 comments:

Post a Comment